FIFA ya Sepp Blatter yafanya alicho takiwa kupewa Pele.
FIFA ya Sepp Blatter yafanya alicho takiwa kupewa Pele.
Akiongea baada ya kupokea zawadi hiyo ya mpira wa dhahabu, ambao umeanzishwa kwa mara ya kwanza, Pele alisema "sasa naona ndoto yangu imekamilika, kwani nimekuwa na wivu kuona wengine wakitunukiwa na hivyo kwa sasa nina kombe vyote nilivyo kuwa navihitaji"
Sepp Blatter ambaye ni rais wa shirikisho la mpira wa miguu FIFA akimsifu Pele alisema" Hakuna mchezaji ambaye amemfikia Pele katika historia ya mpira wa miguu duniani.
"Amefunga magoli zaidi ya alfu moja na kuwafanya watu wapende mchezo wa mpira wa miguu pote duniani na kwa uwezo wake wakusakata soka, na ni mchezaji wa karne ya 20"
Pele hakuweza kupata zawadi hii ya mpira wa dhahabu kwa kuwa mchezaji bora wa dunia enzi za uchezaji wake, kwa sababu alikuwa hajawahi kucheza ligi za Ulaya japo alikuwa akitikisa dunia kwa umairi wake wa kusakata soka na kuwanyanyasa mabeki na makipa kugalagala na kurudi nyavuni kuotoa mpira ulio tikisa nyavu.
SAMUEL E'TOO AMWAGA WINO CHELSEA.
Samuel Eto`o akionyesha jezi yake baada ya kusajiliwa kwa mwaka mmoja akitokea kilabu cha Anzhi Makhachkala.
Pen to paper: Eto'o signs the contract in the presence of Chelsea club secretary and director David Barnard
Samuel Eto`o (32) akionyesha jezi ya Chelsea baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja na kilabu hicho cha London
Man United pointi 13 ubingwa wao
![]() |
| Mshambuliaji wa Manchester United, Robin van Persie akiunganisha krosi kuelekea golini kwa Reading katika mchezo uliozikutanisha timu hizo kwenye Uwanja wa Old Trafford, Manchester. Manchester United ilishinda 1-0. Picha na AFP. |
London, England. Manchester United imefungua milango ya kutwaa taji la 20 la Ligi Kuu England baada ya kushinda 1-0 dhidi ya Reading na kuongoza ligi tofauti ya pointi 15, baada ya wapinzani wake Manchester City kuchapwa 2-0 na Everton ikiwa imebakia michezo tisa kumalizika kwa ligi hiyo.
Mshambuliaji Wayne Rooney alifunga bao pekee la United katika dakika ya 21 baada ya shuti lake kumgonga Alex Pearce na kujaa wavuni. Hilo ni bao la 12 la Rooney katika ligi linaloifanya Manchester Utd sasa kuhitaji pointi 13 kutwaa ubingwa wake wa 20.
Everton imepanda hadi nafasi ya sita baada ya kuichapa Manchester City kwa mabao ya Leon Osman na Nikica Jelavic.
Nayo Aston Villa imepanda juu kwa pointi sita kutoka mkiani baada ya kushinda 3-2 dhidi ya Queens Park Rangers. Arsenal imejiweka vizuri katika mbio za kuwani nne bora baada ya kushinda 2-0 dhidi ya Swansea kwa mabao ya Nacho Monreal na Gervinho. Southampton iliiduwaza Liverpool kwa kuinyuka 3-1.
Barcelona, - Cristiano Ronaldo, Luka Modric na Gonzalo Higuain walifunga katika dakika saba za mwisho wakati Real Madrid ilipoichapa Mallorca 5-2 katika La Liga.
Higuain alifunga mabao mawili na Karim Benzema aliongeza kwa Real Madrid inayoshika nafasi ya pili na kupunguza tofauti ya pointi kubaki 10 kwa vinara Barcelona. Ronaldo alifunga bao lake la 27 katika ligi na 43 kwa msimu huu.
Didier Drogba atemwa kikosi cha Ivory Coast
![]() |
Orodha ya nyota hao wa Ivory Coast iliwekwa kwenye tovuti ya Shirikisho la Soka (www.fif-ci.com) bila ya kueleza sababu za kuachwa kwa nyota huyo wa zamani wa Chelsea.
Wachezaji wengine watano waliocheza fainali za Mataifa ya Afrika mwaka huu wameachwa na kocha Sabri Lamouchi akiwemo beki wa Galatasaray, Emmanuel Eboue, kiungo wa Real Zaragoza, Romaric, kipa wa Dijon, Daniel Yeboah, beki wa Paris St Germain, Siaka Tiene pamoja na beki wa Kuban Krasnodar, Igor Lolo.
Messi aizamisha AC Milan
![]() |
Mabao ya Lionel Messi na David Villa yalitosha kuipa Barcelona ushindi mnono wa 4-0 na kuibwaga AC Milan kwa jumla ya mabao 4-2 kwenye Uwanja Camp Nou.
Kwa ushindi huo Barca imeungana na Juventus, Real Madrid na
Galatasaray iliyolazimisha sare 2-2 na Schalke 04 kwenye Uwanja Auf Schalke na kusonga mbele kwa sheria ya bao la ugenini baada ya mchezo wa kwanza kumalizika kwa sare 1-1 hivyo kufuzu kuingia robo fainali.
Messi ameendeleza rekodi yake kwa kufunga mechi 18 mfululizo, baada ya kuifungia Barca katika dakika 5 na 40, kabla ya Villa na Jordi Alba kupachika mabao mengine mawili.
Washambuliaji wa Milan, Stephan El Shaarawy na M'Baye Niang walipoteza nafasi kadhaa za kufunga katika mchezo huo na kuinyima timu mabao.
Tangu mwaka 1994, Milan imeshinda mechi mbili kati ya mara 12 walizokutana na Barca. Ilishinda 1-0 na 2-0 kwenye Uwanja wa San Siro mwaka 2004 na 2013.
| Mmeumia: Ashley Young atoa onyo kali Man City | ||
WINGA wa Manchester United, Ashley Young ametoa onyo kwa Manchester City kuwa hawapaswi kuendelea kuutolea macho ubingwa wa England msimu huu kwani hawawezi kuupata hata wakitumia sayansi ya aina gani. Mchezaji huyo wanawashangaa wapinzani wao kwa kujitutumua wakati wamewapita mbali na kudai kuwa kuwafikia ni ndoto za mchana. Young na kikosi chake cha Manchester United watashuka uwanjani kucheza na Reading leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Old Trafford na wanataka kurudi kwenye kasi yao baada ya kutetereka katika siku za karibuni. Baada ya Man United kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya wiki moja iliyopita, kikosi hicho kilijikuta kikitoka sare ya mabao 2-2 na Chelsea kwenye robo fainali ya Kombe la FA. Kocha Alex Ferguson ana dalili ya kupata ubingwa baada ya kuwapita wapinzani wao Manchester City kwa pointi 12. Sasa nyota wa England, Young anasema kikosi chake kimesheheni watu wenye uzoefu mkubwa kama Ryan Giggs, Patrice Evra, Rio Ferdinand na Wayne Rooney. "Wachezaji hao wameshinda vikombe vingi, sidhani kama kuna kitu kinachoweza kuharibika. "Unapofika kwenye kambi ya Manchester United kwa mara ya kwanza unatembezwa kwenye kabati la vikombe, unaona ni kwa kiasi gani wamejipanga kushinda. Katika klabu hii ushindi ni utamaduni wetu." Wakati kocha wa Manchester City, Roberto Mancini akikiri timu yake ina nafasi finyu ya kufanya vizuri, nyota Gael Clichy yeye ana mtazamo tofauti, amepania kuimaliza Everton ili kuendelea kuwakimbiza Man United. Manchester City imeifunga Everton mara moja tu katika mechi saba walizokutana katika kipindi cha Mancini na jambo hilo linafanya kikosi cha kocha David Moyes kijiamini zaidi. Lakini Clichy anaamini wanaweza kufanya maajabu kama ya msimu uliopita ambapo walikuwa nyuma kwa pointi nane na kuipiku Manchester United siku ya mwisho. "Ukiangalia mambo yalivyo utagundua kuwa hayatofautiani na mwaka jana ambapo tulikuwa nyuma kwa pointi nane huku tukiwa tumebaki na mechi sita, sasa tupo nyuma kwa pointi 12 na tumebakiza mechi 10. Tottenham ambayo inashika nafasi ya tatu itapambana na Fulham kesho Jumapili huku ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa mabao 4-1 na Inter Milan kwenye Ligi ya Europa. Nayo Chelsea itakwaana na West Ham katika Uwanja wa Stamford Bridge kesho Jumapili. Arsenal, ambayo itakutana na Swansea leo Jumamosi itataka kumaliza hasira baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na Bayern Munich wiki hii. |
Rooney kupewa mkataba mpya Man Utd
![]() |
Vyombo vya habari vya England vimetangaza kuwa mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney anatarajiwa kupewa mkataba mpya wa kuichezea timu hiyo kabla ya mkataba wake haujamalizika 2015.
"Suala la mkataba alionao siyo tatizo, tutakaa naye na kujadili, naamini atasaini mkataba mpya,"alisema kocha wa Manchester United kwa mujibu wa gazeti la The Mail.
Wiki iliyopita vyombo vya habari vya Uingereza viliripoti kuwa kocha Ferguson anataka kumuacha Rooney baada ya kumuacha katika kikosi cha kwanza cha Man U kilichoanza katika mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid wiki iliyopita.
Rooney (27), katika mechi hiyo dhidi ya Real Madrid aliingia katika dakika 73 na alishindwa kuisaidia timu yake kwani ilichapwa mabao 2-1 na Real Madrid na hivyo kutolewa katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kwa ushindi iliopata Real Madrid ilitinga hatua ya robo fainali kwani katika mechi ya kwanza iliyochezwa kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.
Hata hivyo Ijumaa iliyopita kocha Ferguson alifuta tetesi za kuwa Rooney anaondoka Man U, ambapo alisema,"Rooney tutakuwa naye msimu ujao, hayo ni maneno yangu."
Magazeti mengi ya Uingereza jana yaliandika taarifa mbalimbali ambazo zinaonyesha kocha Ferguson anamtetea Rooney huku akiongelea ubora wa hali ya juu alionao Rooney.
Pia magazeti hayo yaliandika kuhusu uamuzi wa kocha Ferguson kuacha kumuanzisha Rooney katika mechi dhidi ya Real Madrid huku kocha Ferguson akisema ulikuwa sahihi kutokana na mbinu aliyokuwa akitumia.
Alisema,"katika klabu yetu ya Mamchester United hatutaki wachezaji wazuri waondoke, Rooney ni kama Paul Gascoigne au Bobby Charlton katika klabu yetu."
Kocha Ferguson alisema,"Rooney mwaka huu alisumbuliwa kwa kuwa, mgonjwa, majeruhi na hakuwa vizuri kucheza mechi nzima, lakini ameweza kufunga mabao 14, najua atamaliza msimu akiwa amefunga mabao 20 sina wasiwasi na hilo."(Daily Mail).
Real yaitupa nje Man U
![]() |
| Beki wa Manchester United,Nemanja Vidic (kushoto) akiwania mpira na kipa wa Real Madrid,Diego Lopez wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa hatua ya 16 bora mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Old Trafford,Manchester. Real ilishinda 2-1. |
Real Madrid imefuzu kuingia robo fainali ya Ligi ya Mabingwa baada ya kuwachapa wachezaji 10 Manchester United mabao 2-1 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Old Trafford.
Real ilipata mabao yake kupitia kwa Luka Modric na Cristiano Ronaldo na kufuta makosa ya Sergio Ramos aliyejifunga mwenyewe kwenye mchezo huo, ambapo Luis Nani alitolewa nje kwa kadi nyekundu.
Nahodha wa Real Madrid, Ramos alijifunga mwenyewe katika dakika 48, wakati akijaribu kuzuia krosi ya Nani na kumpoteza kipa wake Lopez kabla ya kujaa wavuni.
Manchester United walipata pigo katika dakika 57, baada ya kiungo wake Nani kuonyesha kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya beki wa Real, Arbeloa.
Kitendo cha kutoka mchezaji Nani na kuingia Luka Modric kuliirudisha Real mchezoni na katika dakika 66 walisawazisha bao hilo kwa shuti kali la Modric kabla ya Ronaldo kuipa Real bao la ushindi dakika 69 akimalizia vizuri krosi ya kutoka kwa Higuain.
Ronaldo baada ya kufunga bao lake 118 katika michezo 292 aliyoicheza Real hakushangilia kwenye Uwanja wa Old Trafford.
Manchester United waliamka na kuanzisha mashambulizi mengi golini kwa Real, lakini kipa wa Lopez alikuwa kikwazo kikubwa kwao.
Katika mchezo mwingine uliofanyika Uwanja wa BVB, wenyeji Borussia Dortmund waliutumia vizuri uwanja wao wa nyumbani kwa kushinda magoli 3-0 dhidi ya Shakhtar Donetsk.
Michuano hiyo inaendelea leo kwa Juventus kuivaa Celtic na Paris Saint-Germain dhidi ya Valencia.
'Thamani ya mguu wa Messi pauni 3.5mil'
![]() |
Sanamu ya dhahabu yenye thamani ya pauni 3.5 milioni iliyotegenezwa mithiri ya mguu wa kushoto wa Lionel Messi ikiwa na uzito wa kg 25 na urefu wa cm 25 na upana cm 28, ilionyesha kwa mara ya kwanza jana Tokyo.
Mguu wa dhahabu wa Messi umetegenezwa na sonara Ginza Tanaka kwa lengo la kumpongeza mchezaji huyo aliyeteuliwa kwa mara nne mfululizo kuwa mwanasoka bora wa dunia. (bbc)
Waarabu watenga fedha kuinunua Arsenal
![]() |
WAFANYABIASHARA matajiri kutoka Mashariki ya Kati wamejitokeza na kutangaza ofay an kuinunua na kuimiliki klabu ya soka ya Arsenal.
Gazeti la The Telegraph limetangaza mwisho wa wiki bila kuwataja wamiliki hao kuwa wametoa ofa ya pauni biioni 1.5 ( dola 2.3 bilioni) kwa umiliki kamili wa klabu hiyo ya London.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, hiyo ni ofa kubwa kuwahi kutengwa kwa klabu yoyote ya soka duniani.
Ofa hiyo inatarajiwa kutolewa ndani ya wiki chache zijazo, ambako wanunuzi hao wana mpango wa kumwondoa mmiliki mwenye hisa nyingi, raia wa Marekani Stan Kroenke, linaeleza gazeti hilo.
Wawekezaji hao wanatajwa kutoka Qatar na Falme za Kiarabu, kwa mujibu wa The Telegraph.
Tayari wawekezaji hao wamewekwa wazi nia yao ya kuwekeza fedha za kutosha za kusajili wachezaji wapya ili kuibadili klabu hiyo na kuifanya moto wa kuotea mbali barani Ulaya na kote duniani.
"Timu ya wawekezaji inataka kuiona Arsenal inazidi kuwa mojawapo ya klabu kubwa Ulaya, hasa ikizingatiwa ukweli kwamba kwa sasa imeporomoka na kuondoka katika orodha hiyo," gazetim hilo limevikariri vyanzo vya habari.
Wawekezaji hao wanaeleza kuwa wanataka kuwa wanataka kushusha bei ya tiketi ya klabu hiyo kwenye Uwanja wa Emirates pia wanatarajia kurejesha mafanikio yaliyopatikana zama za Highbury, uwanja wa zamani wa klabu hiyo.
Endapo hilo litafanyika, hatma ya kocha wa sasa, Arsene Wenger haijulikani, ingawa vyanzo vingine vinaeleza kuwa wamiliki hao wanaheshimu mchango wake katika soka, kiasi kwamba wanataka kumbakisha klabuni hapo, limeeleza The Telegraph.
Huo utakuwa uwekezaji mwingine katika michezo kutoka matajiri wa Mashariki ya Kati katika miaka ya karibuni.
Tayari, klabu ya Manchester City inamilikiwa na matajiri kutoka Abu Dhabi tangu mwaka 2008, wakati matajiri wa Kuwait' wa familia ya al-Hasawi walinunua klabu iliyowahi kutamba Ulaya, Nottingham Forest mwezi Julai mwaka jana. Klabu ya Paris St Germain ya Ufaransa na ile ya Malaga ya Hispania zinamilikiwa na matajiri wa Qatar.
Suarez apiga tatu, Liverpool ikiua
![]() |
Mshambuliaji Luis Suarez kwa mara ya pili anafunga mabao matatu katika Ligi Kuu na kupanda kileleni kwenye orodha ya wafungaji akiingoza Liverpool kushinda 4-0 dhidi ya Wigan Athletic.
Suarez, ambaye katika msimu huu amekuwa akicheza kama mshambuliaji pekee wa Liverpool sasa amefikisha mabao 21 akiwa mbele kwa magoli mawili kwa mshambuliaji wa Manchester United, Robin van Persie.
Baada ya Stewart Downing kuipa Liverpool bao la kuongoza la mapema dhidi ya Wigan, Suarez alithibisha ubora wake kwa kufunga mabao tatu kwa mara nyingine kama alivyofanya dhidi ya Norwich City.
Suarez alifunga bao la kwanza kwa shuti la mguu wa kushoto lililompita kipa Ali Al-Habsi katika dakika18, alifanya matokeo hayo kuwa 3-0 katika dakika 34, kwa kufunga bao kwa mpira wa adhabu uliomgonga beki na kuingia wavuni kabla ya kuhitimisha kwa kufunga bao lake la tatu akimalizia kwa umakini pasi mzuri ya Glen Johnson.
Msimu uliopita Suarez alikuwa kwenye wakati mgumu baada ya kufungiwa kucheza mechi nane na FAkwa madai ya kutoa maneno ya ubaguzi kwa beki wa Manchester United, Patrice Evra pamoja na kushitumia kuwa na tabia ya kujirusha, msimu huu nyota huyo wa Uruguay anaonekana kama atawanyamazisha wapinzani wake kutokana na kiwango anachokionyesha.
Suarez kwa sasa anakaribia kutwaa tuzo ya Kiatu cha Dhababu na kocha wake Liverpool, Brendan Rodgers anaamini nyota huyo anastahili kupata tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka.
"Ni mchezaji anayejituma," Rodgers alimzungumzia nyota huyo wa zamani wa Ajax Amsterdam. "Si tu kama ananjaa ya mafanikio, lakini ni mtu anayejitoa.
Kocha huyo hakusita kuzungumzia kuhusu kushindwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu ujao kama kunaweza kusababisha Suarez kuondoka Anfield.
"Suala hilo halina uhusiano wowote na Luis, ni matumaini yangu ataendelea kukaa hapa,� alisema Rodgers.
"Ni kawaida kwa mchezaji wa kiwango kutamani kitu kama hicho, lakini tumekuwa kwenye mazungumzo kila wakati na Luis pamoja na wakala wake kwa wiki kadhaa na ameonyesha kwamba ataendelea kubaki hapa.
�Ni vigumu kusema Ligi ya Mabingwa si muhimu kwa sababu wachezaji bora wanataka kucheza mashindano ya kiwango hicho. Mashabiki wanampenda, naye anaupenda mji wa Liverpool, ni matumaini yetu tutakuwana mafaniko mazuri wote katika siku za usoni."
Messi avunja tena rekodi
![]() |
Mshambuliaji wa timu ya Barcelona, Lionel Messi amevunja rekodi ya mwaka 1930 juzi baada ya kufunga bao katika mechi ya 17 mfulululizo katika Ligi Kuu ya Hispania wakati Barcelona ilipoibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Deportivo La Coruna.
Katika mechi hiyo, Messi ambaye ni mchezaji bora wa dunia alitokea benchi na kufunga bao la pili katika dakika ya 88 wakati huo tayari Alexis Sanchez alikuwa ameishaifungia Barcelona bao la kwanza katika dakika ya 38.
Kwa mujibu wa klabu ya Barcelona, Messi amevunja rekodi ya mwaka 1930 ya mshambuliaji wa Poland, Teodor Pewterek aliyefunga mabao 22 katika mechi 16 mfululizo akiwa na klabu ya Ruch Chorzow.
Barcelona yaitamani AC Milan
Kocha wa muda wa Barcelona, Jordi Roura amesema wataingia uwanjani kesho kucheza mechi ya marudiano ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya AC Milan huku wakijiamini.
Katika mechi ya kwanza iliyozikutanisha timu hizo mjini Milan, timu ya Barcelona ilichapwa mabao 2-0 hivyo wanataka kusawazisha mabao hayo na kuongeza ili kutinga hatua ya robo fainali.
"Tumeisha fahamu tutakavyocheza dhidi ya AC Milan na wao ndiyo wanavyotaka sisi tucheze, hatutakubali kuruhusu bao, nitafanya mabadiliko kidogo katika kikosi chetu,"alisema Roura.
Alisema,"Alexis Sanchez anafanya vizuri katika ligi anaweza kucheza katika mechi ya kesho, pia Xavi ambaye alikuwa majeruhi hivi sasa anafanya mazoezi na nitaangalia kama atacheza, bado sijapanga kikosi." (Goal).
SAMIR NA PHILIP KOTEY KUWANIA UBINGWA WA AFRIKA UZITO WA MIDDLE
Nchi ya Ghana iko katika hekaheka na bashasha za mapambano kadhaa ya ngumi mwezi wa Machi tarehe 30 wakati ubingwa maarufu wa middle weight utakapo gombaniwa na mabondia Issah Samir na Philip Kotey. Wawili hawa ni maarufu sana katika tasnia ya ngumi nchini Ghana na barani Afrika kwa ujumla. Watakutana wakati wanapogombea mkanda wa IBF AMEPG uzito wa middle.
Musiki wa aina ya Tangle unahitaji watu wawili kuucheza na ndivyo hivyo miamba hii miwili itakapokutana kwenye "musiki wa masumbwi" ulingoni wakati kila mmoja wake atakapoonyesha ulimwengu kuwa yeye ndiye bondia maarufu zaidi katika bara la Afrika uzito wa middle.
Pambano hili linaandaliwa na GoldMike Boxing Promotions Syndicate, kampuni inayoongozwa na bw. Michael Tetteh pamoja na kigunge mmoja wa biashara za vyalula vilivyokaushwa wa Ghana bw. Henry Many-Spain ambaye pia ni Mamamu wa rRis wa IBF Africa idara ya fedha.
Hivyo siku ya Machi 30, miamba hii miwili itakutana katika mpambano uliopewa jina la “Watoto wa Nkrumah” jina lilaloheshimika sana katika nchi ya Ghana kutokana na Rais wake wa kwanza Mh. hayati Kwame Nkrumah!
Nchi ya Ghana imejitokeza kuwa maarufu katika michezo na inajizatiti kuendeleza michezo yote hususan mpira wa miguu na ngumi. Ni nchi ambayo imeshawahi kutoa mabingwa wengi wa dunia kama kina Azumah Nelson na Ike Quartey ambao walikaa na mataji ya ubingwa ngumi kwa iaka kadhaa na kulitangaza vyema bala la Afrika.
Sasa ni juu ya miamba hii miwili kuafuata nyayo za akina Azumah Nelson, Ike Quartey, Joseph Agbeko na wengine wengi!





















No comments:
Post a Comment