KARIBU KATIKA YOUNGSTAR BLOG.ILI KUWEZA KUTANGAZIWA KATIKA BLOG HII WASILIANA NA NUMBER 0772649868








menu

Search This Blog

Burudani



                                                                                                                                                                      


Keisha agida haja ndogo
Keisha
LONDON, ENGLAND
MIONGONI mwa mashairi maarufu ya mwanamuziki, Keisha ni kujisifu kuwa kila aamkapo asubuhi hupiga mswaki kwa kutumia kilevi ghali aina ya Jack Daniel.

Lakini vituko anavyoimba haviishii kuwaburudisha mashabiki wake, kwani hata katika maisha yake ya kawaida amekuwa akifanya vituko na hapa anasimulia jinsi asubuhi moja alivyojikuta akinywa mkojo wake.

Keisha mwenye umri wa miaka 25 anasema: �Niliambiwa ukinywa mkojo wako unajikinga na maradhi mbalimbali, nilitaka kuwa na afya njema hivyo nikaupokea ushauri huo na asubuhi moja baada ya kujisaidia katika kopo niliunywa.�

Mwanamuziki huyo anasema aliamua kulirekodi tukio hilo na kuliingiza katika �documentary� yake iitwayo �Keisha: My Crazy Beautiful Life� ambayo itatoka hivi karibuni.
                                                                                                                                                                 

Ray aanzia mwaka uswahilini

MWIGIZAJI na mtayarishaji mahiri wa filamu za Bongo, Ray, ameufungua mwaka kwa staili yake baada ya kuzindua filamu mpya katika shule ya msingi Buguruni Malapa, hiyo ni shule maalumu kwa ajili ya watoto viziwi.
Ray aliwatembelea watoto hao na kuongea nao kisha kutoa zawadi mbalimbali kwao na kufurahi nao kwa kuelezea ujio wa filamu yake hiyo mpya ya Waves Of Sorrow.
Amedai kuwa anaamini kuwa wateja wake wengi ni watu wa hali ya kawaida jambo linalomfanya kuwa nao karibu na kuwatembelea walipo kama alivyofanya Alhamisi iliyopita shuleni hapo.
"Nimechagua hapa kuwa ni sehemu ya uzinduzi wa filamu yangu ya Waves Of Sorrow, nawarudishia shukrani zangu kwao kwa kuniunga mkono katika kazi zangu ninazozifanya siwezi kuwafikia wote lakini pale ninapopata wasaa nakuwa mwepesi kufika kwa jamii," alisema Ray.
Ray amekuwa na utamaduni wa kuwatembelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu kila anapotoa filamu zake.
Katika filamu hiyo amewakutanisha wasanii wa kike wanaofanya vizuri wakiwemo Nesh Mohamed na Rose Ndauka.
                                                                                                                                                                   

Lulu: Mimi siombi msaada

LULU ambaye kwa sasa yupo uraiani kwa dhamana huku kesi yake ya tuhuma za kuua bila kukusudia ikiendelea, amesema kuwa hajafungua taasisi yoyote wala kuomba misaada kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.
�Nasikia tu kwa watu eti sijui ninataka wasanii waigizaji kwa ajili ya taasisi yangu, mara nimetoa namba ya simu watu wanichangie ili nitengeneze filamu, sijafanya kitu kama hicho na wala siwezi nahitaji kutulia na kuangalia mambo yangu,� alisema.
Hivi karibuni kupitia facebook kumeonekana akaunti inayotumia picha na majina ya Lulu kwa kuwaomba wadau wa filamu wamchangie fedha kwa njia ya m-pesa na tigo-pesa.
Lulu anatuhumiwa kuhusika na kifo cha aliyekuwa msanii wa filamu, Steven Kanumba, kilichotokea mwaka jana.
                                                                                                                                                                   

Mama Kanumba atoa kitu chake

FLORA Mtegoa ambaye ni mama mzazi wa aliyekuwa mwigizaji wa filamu za Bongo, Steven Kanumba (marehemu sasa), ameigiza filamu ya Without Daddy akiwa na watoto na wasanii walioshiriki katika filamu ya Bigg Daddy ya marehemu Kanumba.
Mama Kanumba ambaye amedai kuwa filamu hiyo ni mwendelezo wa filamu ya mwanaye na kwamba baada ya filamu hiyo hataigiza tena.
�Nimeigiza katika filamu ya Without Daddy katika kuonyesha uwezo katika uigizaji, lakini sidhani kama naweza kuigiza filamu nyingine tena, ni kazi ngumu na inahitaji muda sana. Pia nisingependa kuwa mwigizaji wa moja kwa moja,� anasema Mama Kanumba.
Katika filamu hiyo nyota walioshiriki ni Cathy Rupia, Ben Blanco, Muhogo Mchungu, Bi. Mwenda, Patcho Mwamba �Tajiri�, Othuman Njaidi �Patrick�,Wastara Juma na wengineo.
                                                                                                                                                                    


King majuto ataka tuzo ya trekta
Mchekeshaji mahiri katika tasnia ya filamu nchini, Amri Athuman 'King Majuto
MCHEKESHAJI mahiri katika tasnia ya filamu nchini, Amri Athuman 'King Majuto' ametoa mpya ya mwaka baada ya kusema kuwa si kama hapendi kushiriki mashindano ya wasanii bora bali utata unakuja katika suala nzima la zawadi.

Majuto anasema kuwa kama atatokea muandaaji na kutoa tuzo bora kwa msanii na yeye akawa mshindi basi lazima ajipangie zawadi.

Mimi umri umeenda sana na nafikiria kustaafu, najua kuna watu ambao wanasema kuwa mimi ni bora, sikatai ni kweli mimi ni bora kwa hiyo ikitokea utoaji wa tuzo na mimi nikawa muigizaji bora zawadi ninayoitaka ni trekta ili nikamalizie uzee wangu kwa kilimo bora na cha kisasa,�anasema King Majuto.

King Majuto msanii mwenye masihara kila anapozungumza na watu amesema kwamba suala la kutaka apatiwe trekta ni kweli wala hatanii kama ambavyo wengi wamemzoea.
                                                                                                                                                                     


Beyonce aondoa nyama uzembe

MIAMI, MAREKANI
MWANAMUZIKI Beyonce ambaye alikuwa akikosolewa kwa unene sasa amepungua na kuweka bayana kuwa alikuwa na wakati mgumu.

Beyonce amepiga picha kwenye jarida la GQ litakalotoka Aprili mwaka huu na anaonekana akiwa mwembamba tofauti na siku za karibuni.

Dada huyo mwenye miaka 31 amesema kuwa alikuwa na kazi kubwa ya kujipunguza unene baada ya kupata mtoto wa kike Blue Ivy mwaka jana.
�Sikupata muda wa kutosha wa kupunguza mwili kwa kuwa nilikuwa na ratiba za shoo mfululizo miezi mitatu baada ya kujifungua.

�Kwa kawaida mimi si mwembamba, huwa ninafanya kazi kubwa kuhakikisha mwili wangu unakuwa wa wastani.

"Nawashauri watu wanaojipunguza kuhakikisha hawazidishi kipimo kwani afya njema ni kitu kizuri."
                                                                                                                                                                  


Hipsi za Alicia Keys zazua maswali

LOS ANGELES, MAREKANI
MARAFIKI wa mwanamuziki Alicia Keys wanashangaa kuona mwanamuziki huyo akiongezeka hipsi kila kukicha wakati umbo lake si hilo.

Mwanamke huyo ambaye ni mke wa Swizz Beatz alikuwa na hipsi za wastani lakini umbo lake la chini limekuwa likiongezeka tangu alipopata mtoto wa kiume.

"Tunashangaa kuona hipsi zake zikiongezeka kila kukicha, labda amefanya upasuaji wa kujiongeza," alisema rafiki mmoja wa dada huyo. Lakini dada huyo ameongezeka uzito tangu alipofunga ndoa na mume wake Swizz.

Alicia alifunga ndoa na Swizz mwaka juzi na wana watoto watano katika familia yao. Alicia ana mtoto mmoja na pia analea watoto wanne wa kambo wa Swizz ambao alizaa na wanawake wanne tofauti.

No comments:

Post a Comment