KARIBU KATIKA YOUNGSTAR BLOG.ILI KUWEZA KUTANGAZIWA KATIKA BLOG HII WASILIANA NA NUMBER 0772649868








menu

Search This Blog

Monday, May 19, 2014


NYUMBA YATEKETEA KWA MOTO JIJINI MBEYA

Wakazi wa eneo la Makunguru jijini Mbeya wakiwa wamesimama nje nyumba iliopo kwenye eneo hilo ambayo imepatwa na dhahma ya kuungua moto na kuteketea kwa mali zote zilizokuwemo ndani ya nyumba hiyo, kutokana na kinachosadikiwa kuwa ni hitilafu ya umeme. Bado haijadhibitika mpaka sasa kama kuna mtu yeyote aliedhurika kwenye tukio hilo lililotokea mchana wa leo jijini humoSehemu ya mali zilizokuwemo kwenye nyumba hiyo zikiwa zimeteketea zote kwa moto huo.

Majirani wakichungulia kupitia dirishani kuona namna moto ulivyoteketeza mali zilizomo kwenye nyumba hiyo.
Wengine walikuwa wakihadhithiana tukio hilo.

DIAMOND MPAKA SASA AONGOZA KURA ZA BET KWA KUNDI LA WASANII WA AFRIKA
Msanii Nasibu Abdul alias 'Diamond Platnumz' kwa sasa anakimbiza katika mchakato wa upigaji kura katika Tuzo za BET 2014 ambapo mpaka saa 10:55 leo jioni alikuwa anaongoza katika kundi lake akiwa na asilimia 75.79 ya kura zote akifuatiwa na Mafikizolo wenye kura asilimia 8.34. na wengine kama jedwali linavyoonesha hapo chini. Tuzo hizo zitatolewa Juni 29 mwaka huu jijini Los Angeles, Marekani.

KUMPIGIA KURA DIAMOND , BOFYA HAPA

Kisha telemka chini hadi utapokuta "BEST INTERNATIONAL ACT: AFRICA" bofya tundu lenye jina lake kisha bofya "VOTE"... kitu na boxi!


Thursday, May 15, 2014

People with albinism: Pillay urges more protection after barbaric killing in Tanzania

UN High Commissioner for Human Rights Navi Pillay.
UN High Commissioner for Human Rights Navi Pillay called Thursday for increased protection for people with albinism, after the barbaric murder of a 40-year-old woman with albinism in north-western Tanzania on 12 May.
“This killing and the terrible circumstances surrounding it sadly demonstrate that the human rights situation of people with albinism in Tanzania and other countries, remains dire,” Pillay said.
According to police reports, Munghu Lugata was brutally murdered Monday night at her home in Mwachalala, a village in Simiyu region, north-western Tanzania. Her attackers chopped off her left leg above the knee, two of her fingers and the upper part of her left thumb, apparently while she was still alive.
These attacks, which are often motivated by the use of body parts for ritual purposes, have claimed the lives of at least 73 people with albinism in Tanzania since 2000. Ms Lugata’s murder is the first reported killing of someone with albinism in Tanzania in 2014.
Pillay welcomed the rapid response of the police, who arrested two local witchdoctors on 13 May.

Chama Cha Utabibu wa Dawa Asilia Tanzania chatoa somo kwa Wanahabari jijini dar

Mlezi wa Chama Cha Utabibu wa Dawa Asilia Tanzania (ATME),Mzee Kingunge Ngombale Mwiru (kushoto), akifungua mafunzo kwa wahariri na waandishi wa vyombo vya habari kuhusu tiba asilia, May 15,2014 katika ukumbi wa mikutano NIMR jijini Dar es Salaam,ambapo amewataka Watanzania kuondokana na imani potofu dhidi ya tiba asili na badala yake watumie ili kupona maradhi mbalimbali yanayowakabili (kulia),Mwenyekiti wa Chama cha Utabibu wa Dawa Asili Tanzania (ATME), Bw.Simba Abdulrahmani.

Lucey Samwel, kutoka kitengo cha Tiba asilia Wizara ya Afya akiwakilisha mada ya sera ya Afya, Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala, pamoja na taarifa mbalimbali zinazohusu Tiba Asilia na udhaifu katika usimamizi wa sheria ya TATM ya mwaka 2002.
UJUMBE MWANANA KUTOKA SIKONGE TABORA

LAPF YAONGEZA WANACHAMA HADI KUFIKIA 20,214

Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF kanda ya Mashariki Bw. Sayi Lulyalya akiwaeleza waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam (hawapo pichani ) kuhusu mafanikio yaliyofikiwa na Mfuko huo ikiwemo kukusanya zaidi ya bilioni 115 hadi kufikia machi 2014 sawa na asilimia 94 ya lengo .kushoto ni Kaimu Meneja Masoko wa Mfuko huo Bi Rehema Mkamba. (Picha na Jojina Misama)
Frank Mvungi-Maelezo
Mfuko wa pensheni wa LAPF umefanikiwa kusajili wanachama 20,214 kufikia mwezi machi 2014 wakati lengo lilikuwa wanachama 15,287 katika kipindi hicho.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Kanda ya Mashariki wa mfuko huo bw. Sayi Lulyalya wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Lulyalya alisema ongezeko hilo ni matokeo ya kuwepo kwa utekelezaji wa sera nzuri zenye kuwajali wanachama wa mfuko huo na jaamii kwa ujumla.
Alisema kuwa mfuko huo umepanga kuongeza wanachama wake hadi kufikia 122,595 kwa kuwa mwitikio wa wananchi kujiunga na mfuko huo umekuwa chanya kwa kiasi kikubwa.
“Tumekuwa na wanachama kutoka sekta binafsi ambao nao wameonyesha mwamko wa kujiunga na uchangiaji wa hiari katika mfuko wetu ikiwa ni sehemu ya kujiwekea akiba “ alisema Lyalya
Katika kutoa elimu kwa umma kuhusu faida wanazopata wanachama wa mfuko huo lyalya alisema wamekuwa wakitoa elimu kwa njia ya redio,Televisheni,Magazeti na na Makongamano.
Naye Kaimu Meneja Masoko wa Mfuko huo Bi Rehema Mkamba alisema kuwa Mfuko huo umekuwa ukichangia katika huduma za kijamii ambapo katika mwaka wa fedha 2013/2014 shilingi milioni 200 zilitengwa kwa ajili ya shughuli za kijamii katika sekta za afya,elimu na kusaidia watu wenye mahitaji maalum.
Katika makusanyo mfuko ulijiwekea malengo ya kukusanya shilingi bilioni 122.7 ambazo ni michango ya wanachama na malimbikizo,ambapo hadi kufikia mwezi machi 2014 mfuko umeweza kukusanya bilioni 155.5 sawa na asilimia 94 ya lengo kwa kipindi hicho.
Wanaharakati Waandamana jijini Dar es salaam Kupinga Utekaji wa Wasichana Nigeria

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi (aliyeshika kipaza sauti) akisoma barua maalumu iliyotumwa kwa ubalozi wa Nigeria nchini Tanzania kuonesha wanaharakati hao kupinga utekaji wa wasichana uliofanyika Nigeria.

Mkurugenzi wa WiLDAF, Dk. Judith Odunga, akizungumza kupinga ukatili uliofanywa kwa wanafunzi wa kike kutekwa na kitendo cha Jeshi la Polisi nchini Tanzania kuzuia maandamano hayo ya wanaharakati.

 Viongozi wakuu wa Mtandao wa Mashirika Huru ya Kijamii (CSOs) wakipokea mabango yenye jumbe anuai za kupinga vitendo vya kikatili vilivyofanywa na wanamgambo wa Boko Haram.

Baadhi ya wanafunzi wa kike na wanaharakati wakiandamana kupinga vitendo vya kikatili vinavyofanywa na kundi la wanamgambo wa Boko Haram. Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA