KARIBU KATIKA YOUNGSTAR BLOG.ILI KUWEZA KUTANGAZIWA KATIKA BLOG HII WASILIANA NA NUMBER 0772649868








menu

Search This Blog

Thursday, May 15, 2014

LAPF YAONGEZA WANACHAMA HADI KUFIKIA 20,214

Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF kanda ya Mashariki Bw. Sayi Lulyalya akiwaeleza waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam (hawapo pichani ) kuhusu mafanikio yaliyofikiwa na Mfuko huo ikiwemo kukusanya zaidi ya bilioni 115 hadi kufikia machi 2014 sawa na asilimia 94 ya lengo .kushoto ni Kaimu Meneja Masoko wa Mfuko huo Bi Rehema Mkamba. (Picha na Jojina Misama)
Frank Mvungi-Maelezo
Mfuko wa pensheni wa LAPF umefanikiwa kusajili wanachama 20,214 kufikia mwezi machi 2014 wakati lengo lilikuwa wanachama 15,287 katika kipindi hicho.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Kanda ya Mashariki wa mfuko huo bw. Sayi Lulyalya wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Lulyalya alisema ongezeko hilo ni matokeo ya kuwepo kwa utekelezaji wa sera nzuri zenye kuwajali wanachama wa mfuko huo na jaamii kwa ujumla.
Alisema kuwa mfuko huo umepanga kuongeza wanachama wake hadi kufikia 122,595 kwa kuwa mwitikio wa wananchi kujiunga na mfuko huo umekuwa chanya kwa kiasi kikubwa.
“Tumekuwa na wanachama kutoka sekta binafsi ambao nao wameonyesha mwamko wa kujiunga na uchangiaji wa hiari katika mfuko wetu ikiwa ni sehemu ya kujiwekea akiba “ alisema Lyalya
Katika kutoa elimu kwa umma kuhusu faida wanazopata wanachama wa mfuko huo lyalya alisema wamekuwa wakitoa elimu kwa njia ya redio,Televisheni,Magazeti na na Makongamano.
Naye Kaimu Meneja Masoko wa Mfuko huo Bi Rehema Mkamba alisema kuwa Mfuko huo umekuwa ukichangia katika huduma za kijamii ambapo katika mwaka wa fedha 2013/2014 shilingi milioni 200 zilitengwa kwa ajili ya shughuli za kijamii katika sekta za afya,elimu na kusaidia watu wenye mahitaji maalum.
Katika makusanyo mfuko ulijiwekea malengo ya kukusanya shilingi bilioni 122.7 ambazo ni michango ya wanachama na malimbikizo,ambapo hadi kufikia mwezi machi 2014 mfuko umeweza kukusanya bilioni 155.5 sawa na asilimia 94 ya lengo kwa kipindi hicho.

No comments:

Post a Comment