KARIBU KATIKA YOUNGSTAR BLOG.ILI KUWEZA KUTANGAZIWA KATIKA BLOG HII WASILIANA NA NUMBER 0772649868








menu

Search This Blog

Friday, March 16, 2012

ujenzi kilimani

Ujenzi ‘Botanical Garden’ Kilimani

Written by staryoung bieber //  08/03/2013  //  Habari  //  No comments
Viongozi wetu wote watatu: Dr.Shein, Maalim Seif, na Balozi Seif wanapenda kuimba nyimbo ‘uhifadhi wa mazingira’; na wakati mwengine waajivuna ‘zanzibar ya kale’ – zanzibar ilivyokuwa.
Inasikitisha sana kuona kuwa ujenzi umeanza pale Botanical Garden pale Kilimani/Migombani. Inashangaza kuwa Dr.Shein hajauona ujenzi huu wala Seif Ali Iddi au maalim Seif ilhali kuwa wanapita kila siku hapo zaidi ya mara tatu kwa siku. Ujenzi unafanywa mbele ya macho yao.
Hivi kweli hawajaona au hawataki? Hivi kweli Dr.Shein, ziara yako ya juzi ya Mkoa Mjini Magharib, hujaona ujenzi huu – ambao, by any definition, hauruhusiwi kwa kuzingatia kuwa hilo ni eneo ‘ama tuliite reserved area au preserved area’, tena ni eneo nyeti sana (kituo cha polisi ndio mpaka wa ukuta).
Kihistoria eneno hili lilikuw ana miti mingi sana ya akila aina, kutoka kila kona ya dunia, na ni eneo pekee kwa Afrika Mashariki (la kwanza kuwa na botanical garden).
Leo yote imefyekwa, na sasa inamegwa kidogo kidogo na kuanza kujengwa. Alianza Naushad, halafu kituo cha Polisi, sasa nani sijui amepewa.
Itakavyokuwa huyu anayejenga hapa ama ni CCM au mtu mkubwa serikalini, au ni mtu wa biashara anayeiunga mkono CCM 100%.
Hivi kweli Dr.Shein tukuamini vipi, akifanya Farid, Azan, Msellem n.k tunawaweka ndani, wakifanya wengine lakini wakihujumu mali ya umma, unawabeba kichwani kwa raha zako.
Hivi kweli wakubwa wote serikalini mnataka kusema hamjaona hapo kuwa panajengwa ilhali haparuhusiwi kujengwa? Hii ni njia kuu, wakubwa wote takriban 95% wanapita njia hii go-and-from. Basi hakuna hata mmoja aliyeweza kusema kitu?
Iko wapi Idara ya Ardhi, au ile Mipango Miji? Juzi juzi tu, Idara hizi mbili walikwenda kuvunja nyumba za watu kule Kwarara/au sijui kunaitwa wapi eti “wamevamia” ardhi just kwa sababu “hamkuelewana vizuri kimaslaji”. Huyu hapa mnamuacha kama alaivyo, kwa sababu……..???
Dr.Muhammed Juma – Mkurugenzi wa Mipango Miji, na January Fussi – kweli hamuoni haya, yanayofanyika hapa Kilimani/Migombani botanical garden?? Mnawavunjia nyumba maskini ya Mungu, hawa mnawawacha. Dr.Muhammed, ujue wewe kuwa unatoka mbali,umehangaika sana mpaka umefika hapo (Habari za Paris balahau…..est que tu….?)
Pale Mambomsiige, na ile open space, mmempa mtu anajenga hoteli, pamoja ya kuwa wakaazi wa mji mkongwe wamekataa tena kwa petition, mwisho Dr.shein anasema kuwa serikali haihojiwi kwa kuuza chake. Sasa, na wengine watauza ardhi, gari, na nyumba za serikali and don’t question please. Mimi nahisi kuuza mali za serikali ndio inahitaji kuhijiwa zaidi kuliko kuuza mali ya mtu binafsi?
Tunaomba tuone hatua imechukuliwa. Kinyume chake, a wengine tutaomba viwanja pale Mnazi Mmoja na kuanza kujenga.

No comments:

Post a Comment