JOZANI forest - Zanzibar
Ukiwa unapenda wanyama pori basi hata kama utaenda visiwani utatamani
uwaone hata kama ni wadogo na wachache. Visiwa vya Zanzibar, vimejaaliwa
kuwa na aina ya pekee ya mbega ambao wanapatokana Visiwani humo tu. Hao
ni Zanzibar Red colobus monkeys - Mbega wekundu wa Zanzibar. Na msitu
wa Jozani ndio eneo mahususi lililotengwa kuwahifadhi na kuwapa fursa
wengine kuja kuwaona viumbe hawa adimu. Tofauti na misitu na hifadhi
nyingi za Hapa nchini, Msitu wa Jozani mgeni hutembea kwa miguu kuwasaka
Mbega walipo. inategemea na muda na hali ya mazingira kwani unaweza
tembea kwa masaa kadhaa ili kuwapata. Siku hii ilituchukua muda mfupi
sana kuwaona kwani ilikuwa ni mida ya jioni na walikuwa wamesogea karibu
kabisa na geti la kuingilia kwenye hifadhi.
Tulilikuta kundi kubwa la mbega likiwa kwenye eneo lijulikanalo kama
restaurant. Walikuwa ni kundi la mbega wapatao 30 hivi, wakubwa na
wadogo - majike na madume. Tofauti na nyani, Mbega wao sio waoga wa
binadamu na wanaweza kumsogelea mtu bila wasiwasi au wakakuruhusu
ukawasogelea wao bila wao kuwa na shaka na wewe.




No comments:
Post a Comment