KARIBU KATIKA YOUNGSTAR BLOG.ILI KUWEZA KUTANGAZIWA KATIKA BLOG HII WASILIANA NA NUMBER 0772649868








menu

Search This Blog

Wednesday, May 14, 2014

MUALIKO WA SHEREHE ZA SIKU YA MAKUMBUSHO DUNIA NA UFUNGUZI WA UKUMBI WA KUDUMU WA SANAA.
Kila Tar 18 Mei Jamii husherekea siku ya Makumbusho Duniani, hapa Tanzania sherehe hizi Kitaifa zitafanyika Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar Es Salaam. Katika siku hii muhimu, Makumbusho ya Taifa inatarajia kuufungua rasmi Ukumbi wa Maonesho ya kudumu ya Sanaa.
Kutokana na umuhimu wa siku hii Makumbusho ya Taifa inawakaribisha Watanzania wote kutembelea Makumbusho ya Taifa ili kujifunza mambo mbali mbali kupitia vitu na naarifa zinazothaminiwa na jamii zilizo hifadhiwa na Makumbusho.
Ufunguzi unatarajiwa kuanza saa 10 :00 jioni na utapambwa na Kikundi cha Sanaa cha GODYKAOZYA & THE TONGWA ENSEMBLE kutoka Bagamoyo.
Kuanzia Tar 16 - 18 watu wote watapatiwa huduma za Kimakumbusho BURE. Usikose fursa hii Muhimu kwa ongezeko la uelewa wako juu ya nchi yako.
Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni ipo Posta mtaa wa Shaaban Robert mkabala na chuo cha usimamizi wa Fedha(IFM)Karibuni sana.
SIXMUND J. BEGASHE
MRATIBU WA MAANDALIZI

No comments:

Post a Comment